JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA SINGIDA YATIMIZA AHADI .

 

Mwenyekiti wa Jumiya ya wazazai Mkoa wa Singida Bertha Nakomolwa akiongoa na wazazi wa kata ya Misuna kabla ya kukabidhi madawati aliyokuwa ameahaidi kutoa katika shule ya Msingia Kimpungua.




Mjuimbe wa Baraza  Taifa kupitia jumuiya ya wazazi mkoa wa Singida Mhe.Valelian  Kimambo akitoa wito kwa wazazi juu ya mmomonyoko wa maadili unaoendelea sasa hiku akitoa taadhali.


Singida

 Katika kuhakikisha  wanafunzi washule ya msingi wanakuwa  katika mazingira bora na kuondokana na changamoto ya uhaba wa madawati,vyumba vya madarasa na miundombinu mingine,jumuiya ya wazazi Mkoa wa Singida ya chama cha mapinduzi CCM imekabidhi madawati katika shule ya Msingi Kimpungua Manispaa ya Singida.

 Elimu ni kati ya Sekta ambayo Serikali imehakikisha inaipakipaumbele kwa kuboresha miundombinu yake,jumuiya ya wazazi nao wakaamua kuunga mkono juhudi hizo za Serikali. 

Mwemyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa Betha Nakomolwa anasema wao kwa sasa wamechagua  kuchangia madawati katika shule ya Msingi kimpungua lengo likiwa ni kutaka wanafunzi waketi wote pindi wanapokuwa wanajifunza.

 Hata hivyo baada ya kupokea madawati hayo uongozi,waalimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo wamefurahishwa na kitendo hicho kwani umedhihirisha kuwa jumuiya hiyo ni walezi.

 Akizungumza na kutoa shukrani kwaniaba ya uongozi na wanafunzi mwalimu mkuu wa shule hiyo Tabu Issa ameiomba jumuiya hiyo kuendelea kushirikiana na uongozi wa shule katika malezi ya watoto.

 

Insert............Mwalimu Mkuu wa Shule.

 

 


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments