Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida Sipha Mwanjala akitoa taarifa ya miezi mitatu ya Takukuru Mkoa wa Singida kwa wanahabari.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Singida imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 136 kwenye miradi ya maendeleo iliyokuwa ikitekelezwa mkoani hapo.,
Akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha Aprili hadi juni mwaka huu kwa waandishi wa habari, Mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Singida Sipha Mwanjala amesema fedha hizo zimeokolewa baada ya ufuatiliaji wa taasisi hiyo katika miradi ya maendeleo.
Akizungumzia juu ya mashitaka Mwanjala amesema kuwa Malalamiko 55 yalipokelewa kwa kipindi hicho ambapo malalamiko 20 yalihusu vitendo vya rushwa na malalamioko 35 hayakuhusu vitendo vya rushwa .
Aidha katika kuhakikisha wananchi wanapata uelewa kuhusu vitendo vya rushwa kwa lengo la kuzuia vitendo hivyo amesema wanaendelea kutoa elimu katika makundi mbalimbali.
Hata hivyo amesema kuwa Takukuru mkoa wa Singida umeweka
mikakati ya kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu juu ya rushwa huku akiwaomba
wananchi na wadau wengine kutoa ushirikiano kwenye uchunguzi na kutoa ushahidi
mahakamani.
0 Comments