Dkt Sylvestar Rugeihyami akifafanua zaidi juu ya lengo la mafunzo hayo na lengo lake katika Mikoa yote itakayoya bara na visiwani.
Dkt Elpidius Baganda afisa Elimu Mkoa wa Singida akifungua semina hiyo ya siku mbili iliyowakutanisha wakuu wa Shule mabalimabli katika mkoa wa Singida.
Singida
Katika kuhakikisha somo la hisabati linakuwa na ongezeko la ufaulu nchini Serikali imeanzisha mradi unaolenga kuongeza ufaulu wa somo la hisabati hapa nchini katika shule za Sekondari kutokana na somo hilo kuwa na kiwango kidogo cha ufaulu.
Wakuu wa shule za Sekondari mkoani hapa wamekutana kwa pamoja katika semina elekezi ya siku mbili inayotekelezwa na mradi wa COSTECH mradi ambao umelenga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari katika somo la hisabati.
Akizungumza katika Semina hiyo Mgeni rasmi, Afisa elimu Mkoa wa Singida Dkt.Elipidius Baganda amesema moja ya sababu zinazofanya kiwango cha ufaulu wa somo hilo kuwa mdogo ni pamoja na mtazamo hasi.
Aidha akitaja
mbinu mojawapo katika kuinua ufaulu wa somo la hisabati Mwezeshaji kutoka Idara
ya hisabati chuo kikuu cha Dar -es- salaam dkt.Slivesta Rugeihyam amesema ni
mwalimu kuwa rafiki kwa mwanafunzi.
Baadhi ya wakuu
hao wa shule kutoka shule tano za
sekondari kutoka mkoani singida wanasema
kutokana na wanafunzi wengi kuamini kuwa somo la hisabati ni gumu imepelekea
washindwe kufanya vizuri huku wengine wakiamini baada ya semina hiyo ufaulu
utaongezeka.









0 Comments