Sheikh wa wilaya ya manispaa ya Singida,Issa Ramadhan
Simba (aliyesimama) akitoa nasaha zake kwenye kilele cha maadhimisho ya Idd al Adha yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ipembe mjini Singida jana.
Sheikh wa wilaya ya manispaa ya Singida,Issa Ramadhan Simba (aliyepinga magoti wa kwanza mbele) akishiriki maombi kwenye kilele cha maadhimisho ya Idd aL uedhhiya, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ipembe mjini Singida jana.
Katibu wa BAKWATA mkoa wa Singida Burhan Mlau,akitoa nasaha zake kwenye kilele cha maadhimisho ya sherehe za Iddi Al-Udhhhiya (chijo) kwenye uwanja wa Ipembe mjini Singida.
Na Mwandishi Wetu
Akizungumza
kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya sherehe ya Idi al adha (Chija) ya siku tatu, sheikh wa manispaa ya
Singida Issa Ramadhan Simba alisema hivi sasa vijana wengi wamepotoka na
kusahau maadili yaliyo mema.
“Kwa
kweli tuna mmonyoko mkubwa wa maadili hasa kwa watoto wetu tunaongoza kwa
maporomoko hayo mabaya.Tujifunze kutengeneza maadili mema kwa watoto
wetu,ili tuwe na kizazi chema mbele ya safari”,ameongeza.
Amewasihi wazazi/walezi
kupitia Eid hiyo kila mtu atazame au afuatilie nyenendo za watoto wake kama
zinazingatia maadili mema Endepo kuna mtoto anakwenda kinyume basi arekebishwe
mapema.
Pia
sheikh Simba amewataka wakazi wa wilaya hiyo,kuiombea nchi ipite salama kipindi
hiki cha kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa.
Awali
Katibu wa BAKWATA mkoa wa Singida,Sheikh Burhan Mlau,alisema dunia nzima sasa
hivi inaadhimisha sherehe ya Eid al adha Hivyo waumini wanapaswa kuisherehekea
kwa utulivu.
Katika
hatua nyingine,Sheikh Mlau,ametumia fursa hiyo kumshukuru sana Rais Dk.Samia
Suluhu Hassan,kwa uongozi wake ambao pamoja na mambo mengine mazuri,amepelekea
nchi kuwa ya amani na utulivu mkubwa.
Aidha
ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa manispaa ya Singida kujitokeza kuomba nafasi za uongozi kwenye
uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Mlau manispaa ya Singida
imepata ng’ombe 7,000,mbuzi na kondoo 20,000 kutoka nchi za Misri na
Uturuki.Kwa ajili ya maadhimisho ya Eid al adha kwa wakazi wa manispaa ya
Singida.
0 Comments