Aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi
Mkoa wa Singida Stella Mutabihirwa ametoa wito kwa waandishi wa habari kufanya
Kazi zao kwa kuzingatia maadili ya tasnia hiyo kwa maendeleo ya jamii na Taifa
kwa ujumla.
Mutabihirwa ameyasema hayo katika
ofisi ya jeshi la polisi Singida wakati akikabidhiwa cheti cha shukrani kwa
ushirikiano na klabu ya waandishi wa habari mkoani hapa Singpress.
Akikabidhiwa cheti hicho na Mwenyekiti
wa Singpress Elisante John, Mutabihirwa alisema ni vizuri waandishi wakaandika
habari kwa kufuwata vigezo husika ili kuondoka sintofahamu kwa wasomaji.
0 Comments