Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amewaagiza maafisa michezo wote kutoka wilaya zote mkoani Singida kuhakikisha wanarudisha na kutenga maeneo ya michezo mashuleni.
Kauli hiyo ameitoa mjini Singida katika zoezi la ugawaji wa
mipira ya soka mashuleni program inayoratibiwa na Shirikisho la mpira wa
miguu nchini TFF..
Serukamaba amesema kuwa mipira hiyo iliyoletwa na TFF
ikawechachu ya maendeleo ya michezo katika kila Wilaya Mkoani hapa.
Awali akiongea kwa niaba ya rais wa TFF Wallec Karia Mwenyekiti
wa chama cha Soka Mkoa wa Singida SIREFA Hamisi Kitila amesema kuwa mkoa wa
Singida umepokea jumla ya mipira 1000 kwaajili ya Mradi wa FOOTBALL FOR SCHOOLS
Mradi unaotekelezwa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.
0 Comments