Mkuu wa
Wilaya ya Hanang Janeth Mayenga (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Tawi na
BRAC Tanzania Finance Ltd (BFTL) Lucy Mwaikena wakati wa makabidhiano ya mifuko
ya saruji hiyo .
Misaada
mbalimbali imezidi kumiminika kwa waathirika wa mafuriko wilayani Hanang’
mkoani Manyara, safari hii ikiwa ni ,mifuko ya saruji yenye thamani ya
Sh.milioni 25.
Msaada huo umetolewa na kampuni ya BRAC Tanzania
Finance Ltd (BTFL)
inayojihusisha na masuala ya kifedha imewakumbuka
waathiriwa wa Mafuriko ya Katesh Hanang yaliyotokea Desemba mwaka jana.
Mafuriko hayo yaliweza kusababisha familia nyingi
kukosa makazi na kukabiliwa na changamoto kubwa katika ujenzi wa nyumba zao
pamoja na huduma zingine za kijamii.
Meneja wa Mawasiliano BTFL, Emma Mbaga, alisema wanalenga
kuchangia zaidi katika ujenzi na kusaidia kupunguza
baadhi ya gharama inayowakabili waathirika wa
mafuriko.
Alisema saruji ni nyenzo muhimu ya ujenzi ambayo
itakuwa muhimu katika kujenga nyumba, miundombinu na maeneo ya huduma za
kijamii ambavyo vimeharibiwa na mafuriko.
"Katika nyakati za shida, ni muhimu kwa
mashirika na jamii kuja pamoja kushirikiana na kutoa msaada kwa wale
wanaohitaji.
“Tulihuzunishwa sana na maafa na
uharibifu uliosababishwa na mafuriko na matope
huko Katesh ambayo yameathiri wananchi wenzetu wengi,” alisema.
Makabidhiano ya mifuko 1,413 ya saruji yalifanyika
katika Ofisi ya Wilaya ya Hanang’ mjini Katesh na mchango huo na kupokelewa na
Mkuu wa Wilaya ya Kateshi,
Janeth Mayenga.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Janeth Mayenga,
ameishukuru BTFL kwa kuwakumbuka wahanga wa mafuriko na kuwaletea saruji ambayo
itawasaidia katika kujenga miundo mbini ambayo iliharibiwa.
Aidha, ameziomba taasisi zingine ziendelee
kujitolea hata kwa kidogo kwani wananchi bado wanauhitaji mkubwa ili kurejea
katika maisha yao kuwa kama hapo awali.
Brac Tanzania Finance Ltd (BTFL) imeendelea
kujikita katika kusaidia jamii, ukiachilia mbali ni Taasisi ya kifedha ila
imekua mstari wa mbele kutoa misaada kwa makundi mbalimbali.
0 Comments