Bi Tunu Pinda akiongea na akinamama wa Mkoa wa Singida Wilayani Ikungi.
Katibu tawala mkoa wa Singida Dkt Fatma Mganga akiongea machache kabla ya kukata keki maalum ya Harambee ya Madhimisho ya kilele cha siku ya Mwanamke Duniani.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa wilaya ya Singida Mjini Lucia Mwiru akiongea na waandishi wa Habari katika siku ya kilele wilayani Ikungi..
Serikali imeendelea
kuunga mkono jitihada za kimataifa za kukuza usawa wa kijinsia ikiwa ni pamoja
na kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuwa na kizazi chenye usawa wa kijinsia.
Hayo yamesemwa na mama
Tunu Pinda mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda alipokuwa mgeni rasmi katika
kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mkoa wa Singida
yaliyofanyika Wilayani Ikungi.
Tunu alisema serikali
katika kuhakikisha inakuza usawa wa kijinsia imezindua kamati ya ushauri ya
Kitaifa ya utekelezaji wa ahadi za nchi kuhusu kizazi chenye usawa ili kuchukua
hatua za makusudi kushughulikia mifumo kandamizi kwa wananwake.
Awali akizungumza kabla
ya maadhimisho hayo kuanza katibu tawala Mkoa wa Singida Fatma Mganga alisema
wanawake wajitokeze katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwani kuna
mifano ya wanawake wengi ambao waligombea nafasi za uongozi sawa na wanaume na
wakashinda.
Hata hivyo mwenyekiti wa
chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Lusia Mwiru amesema Mkoa wa Singida
unajivunia kuwa na viongozi wanawake ambao wameingia katika vikao vya maamuzi
huku wakifanya kazi kwa weledi.
0 Comments