Mbunge wa jimbo la
Singida Mashariki Miraji Mtaturu ametoa pikipiki mbili kwa lengo la kusaidia
jitihada za kupambana na ukatili wa kijinsia vinavyofanyika katika jamii.
Akikabidhi pikipiki hizo
wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mkoa wa Singida
yaliyofanyika Wilayani Ikungi Mtaturu amesema pikipiki moja itatumiwa na dawati
la polisi Wilaya ya Ikungi na nyingine itatumiwa na ofisi ya ustawi wa jamii.
Ameongeza kuwa hivi
karibuni atakabidhi pikipiki nyi ngine ya tatu kwa Shujaa wa Maendeleo na
Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA wilaya ya Ikungi ili kuwaongezea nguvu katika
kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto.
Hata hivyo Mtaturu
amesema si jambo zuri kwa baadhi ya wananchi kutoa lugha ambazo sio nzuri kwa
viongozi wa serikali.
Naye mbunge wa viti
maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Nusrat Hanje amesema
ni jambo jema kuipongeza serikali kwa kazi inazozifanya kwani sio rahisi
kutatua changamoto zote kwa wakati mmoja.
0 Comments