WANANCHI wanaotumia barabara ya kutoka Singida hadi
Sepuka na Kaselya Wilaya ya Ikungi na
Iramba Mkoa Singida wanalalamika barabara yao imeharibika na mvua na hakuna
hatua zozote zinazochukuliwa na wahusika waliokabidhiwa barabara hiyo mwezi
Oktoba 2023 na Serikali sasa wanaiomba wakala wa barabara Mkoani Singida (TAN
ROADS) kuitegeneza barabara hiyo.
Barabara kuu Singida hadi Ndago na Kizaga kupitia
Sepuka km 77.6 ambayo kampuni ya Henan Higway ilikabidhiwa na serikali iwekewe
lami sasa barabara hiyo kilometer 25 imeharika vibaya baada ya mvua kunyesha
kuanzia mwezi Nov 2023 hadi Mwezi huu march 2024 kuna mashimo marefu katikati
ya barabara ,mahandaki,mifereji katikati ya barabara na pembeni mwa barabara
kuna makorongo mapana magari hayawezi kupita wala kupishana hivyo magari ya
abiria hutumia muda Zaidi ya masaa matatu kutoka Singida hadi Sepuka
na Kaselya.
Madereva na abiria wanaoitumia barabara
hiyo hawaoni sababu ya barabara hiyo kuwa kuwa mbovu muda mrefu kiasi kile bila
ya matengenezo hivyo wameomba TAN ROAD iingilie kati kunusuru hasara wanaoipata
kutokana na ubovu wa barabara hivyo wamesema barabara hiyo sasa inaharibu
magari yao.
Uongozi wa TAN ROAD Mkoani Singida na wale wa TARURA
Ikungi wanakiri barabara hiyo kwa sasa ni mbovu kabisa hata hivyoMeneja TAN
ROAD Mkoani Singida Mhandisi Massama Massama hakuweza kupatikana kuelezea
marekebisho yake lakini taarifa anazo.
Barabara hii ya Singida hadi Sepuka km 17 inangojewa
sana wananchi wa Wilaya za Singida Mjini na Ikungi kusafirisha abiria na
mizingo yao na mazao ya kilimo,mifugo na smaki kwenda kwenye masoko
ndani ya Mkoa na Nje kwa sababu inapita kwenye maeneo yenye mikakati ya kiuchumi.
Kuanzia barabara ya Mwaru hadi Kaugeri inayoungana
na barabara ku ya Singida hadi Sepuka mwezi Aprili magari makubwa ba madogo
yatapita vijijini kuchukua mpunga,mchele,mahindialzeti,
Wavuvi walioko Kaugeri,Mwakanja,Magungumko na
mduguyu na wale waliopo maeneo yenye samaki vijiji vya kata ya Mwaru
wanaitegfemea barabara hiyo kusafirisha bidhaa za samaki kwenda mikoani
barabara ikiwa mbovu namna hii watashindwa kwenda na kasi anayoitaka Rais Samia
ni vema sasa itegenezwe.
Diwani wa kata ya Mwaru Idd Mkangale amasema
barabara ya Singida hadi Sepuka na ile ya Sepuka hadi Kaugeri kupitia Mwaru
mwaka hu itaingizia mapato makubwa Halmashauri na mapato ya kata yake kuingiza
Wilaya ya Ikungi ni maratatu kuliko mapato ya mwaka uliopita kwa sababu mpunga
na samaki ni wengi.
Diwani Makangale amesema wafanyabiashara wa
samaki,mpunga na mchele watakuwa wengi kutoka mikoani hivyo mzunguko wa pesa
katika kata yake utakuwa mkubwa licha ya kuwepo kwa mazao mengime ya kilimo na
mifugo sasa ni vema baraba zitengenezwe.
0 Comments