Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro imewahukumu kifungo cha miaka 30 jela Rayvan Kidandaa maarufu kama Kisasi (23) mkazi wa Turiani Morogoro na wenzake wawili ambao ni Hamisi Athuman (20) pamoja na Paulo Sinenepi (20) wote wakazi wa Turiani kwa kosa la Unyang'anyi wa kutumia silaha.
Watuhumiwa hao walitenda kosa Februari 1, huko katika Kijiji Cha Mjimpya Tarafa ya Turiani ambapo walimvamia mfanyabiashara mmoja maarufu kwa jina la Jombi kwa kutumia silaha aina ya mapanga kisha kumjeruhi vibaya na kimpokonya pesa Tsh Milioni Sita.Kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti mwaka 2022 Watuhumiwa hao walikamatwa na Jeshi la Polisi chini ya mpelelezi wa shauri hilo A/Insp Dominick Deogratius Paschal na kuwafikisha Mahakamani na kuhukumiwa kifungo hicho mbele ya Mh.
0 Comments