Wananchi Wilayani Ikungi Mkoa wa Singida wametakiwa kuacha tabia ya kumaliza kesi za ukatili nyumbani na badala yake wapeleke mashauri hayo katika vituo vya Polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake.
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Mkoa wa Singida, Mrakibu wa Polisi (SP) Brainer John Robert katika shule ya Msingi Ikungi Wakati akiongea na wazazi na watumishi wa Halmashauri wilayani Ikungi, ambapo amewataka viongozi katika nyanja mbalimbali kukemea vitendo vya baadhi ya wananchi kumaliza kesi za ukatili nyumbani bila kuzifikisha katika vyombo vya kisheria.
"Niwaombe viongozi wa Dini kuendelea kufanya doria ya kiroho kwa waumini wenu kwa lengo la kuwalinda na ukatili ambao umekuwa ukiendelea katika jamii zetu ili tupate viongozi wa baadae ambao tumewalea katika mema "alisisiza Sp Brainer.
Naye, Mkuu wa Dawati la Jinsi na watoto Wilaya Singida Mkaguzi wa Polisi Amina Haji Abdallah akitoa elimu ya ukatili kwa watoto hao aliwataka watoto kutoa taarifa kwa walimu na wazazi dhidi ya vitendo vibaya vya ukatili huku akiwasihi kuhakikisha kila mtoto anamlinda mwenzake bila kuogopa.
Mtandao huo wa Polisi wanawake walifanikiwa kutoa elimu pamoja na kutoa mahitaji mbalimbali kwa watoto hao wenye uhitaji maalumu ikiwemo Mashuka 70, Sabuni mifuko 2,Taulo za kike boksi mbili, Mafuta ya kupaka carton 2, Kofia pea 50, Khanga pea 20, Yeboyebo pea 90
Sabuni zakuogea boksi moja, Pipi mifuko 3, Juice carton 9, Biscut boks 3 Pamoja na maji carton 12
Aidha, Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Singida mara baada ya Kufika wilaya ya Ikungi walifika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Thomas Apson aliwapongeza askari hao kwa namna walivyojipanga kuelekea maadhimisho ya siku ya mwanamke dunia yatakayofanyika machi 8, 2023 kimkoa Wilayani Ikungi.
0 Comments