Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amkabidhi Ofisi mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa.
Picha ya pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri 7 wa mkoa wa Singida.
picha na Wenyeviti wa Halmashauri 7 za mkoa Singida
picha na wakuu wa wilaya za mkoa Singida.
Picha na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Singida.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Halima Dendego ameahidi kushirikiana na viongozi wengine na
wananchi wa Mkoa huo kuleta zaidi maendeleo kwa jamii na Taifa na kufanyia kazi
changamoto za wananchi.
Ameyasema hayo wakati
wa makabidhiano ya ofisi na mkuu wa mkoa aliyehamishwa kwenda mkoa wa Iringa
kutoka Singida Peter Serukamba.
Dendego ambaye
amehamishiwa Mkoani Singida akitokea Mkoa wa Iringa amesema anamshuruku Rais
Samia kwa kuendelea kumwamini na kuahidi kuwa ataendelea kufanya kazi
kulitumikia Taifa na kuongeza huwa watumishi wa Singida wajipange kutumia
maarifa katika utendaji ili kupata majibu ya changamoto za wananchi.
Hata hivyo kwa upande
wake aliyekuwa mkuu wa Mkoa Singida Serukamba ambaye sasa ni mkuu wa Mkoa wa
Iringa amesema Mkoa wa Singida uko chini kiuchumi ukilinganishwa na Mkoa
waIringa hivyo amejipanga kwenda kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili Iringa
iendelee kuwa juu zaidi kiuchumi.
Serukamba amesema Mkuu
wa mkoa wa sasa wa Singida Dendego ni mchapakazi na kupitia uzoefu wake katika
uongozi ataleta maendeleo makubwa kwa Mkoa wa Singida.
Halima dendego
amechukua nafasi ya Peter Serukamba aliyehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Iringa.
0 Comments