Katibu tawala mstaafu mkazi wa wilaya ya Manyoni,Doroth Aidan Mwaluko,akitoa nasaha zake kwenye maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Manyoni mjini.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule za msingi na sekondari waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Manyoni.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule za msingi na sekondari
waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano halmashauri ya Manyoni.
VIJANA wa kiume shule za msingi na sekondari wilaya ya Manyoni
mkoani Singida,wameiomba jamii isiwasahau katika kushiriki masuala mbalimbali
ya kijamii,kiuchumi na kiutamaduni.
Ombi hilo limetolewa na vijana wa kiume wa sekondari ya
Kilimatinde na St.John’s zote za wilaya ya Manyoni.Vijana
250 wa kiume na kike kutoka shule ya msingi Kilimatinde na St.John’s,walikutana
pamoja kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Akizungumza kwa niaba ya vijana wa kiume,Silvester
Saniani,alisema kuwa jamii ya sasa imeweka kipaombele zaidi,kwa watoto wa kike
kuliko wa kiume.
Ameongeza kwamba kuanzia ngazi ya familia,shuleni na
maeneo mengine,vijana wa kike wamekuwa wakipewa vipaombe zaidi.
“Kijana wa kiume hata akichelewa kurudi nyumbani, hakuna mtu
anayefuatilia.Ikitokea kwa bahati mbaya kijana wa kiume akijiunga na kundi
lisilo faa,jamii haitachukua hatua yo yote kumrejesha kwenye maisha
salama.Wazazi na jamii,watamwona mwanafunzi ana acha shule,hakuna
atakayejali”,amesema kwa masikitiko.
Mwanafunzi huyo ametumia fursa hiyo kuiomba jamii kwa
ujumla,iungane pamoja kuhakikisha vijana wa kiume wanapewa vipau mbele, kama
inavyotokea kwa vijana wa kike.
Katika kilele cha maadhimisho hayo,wanafunzi walipata fursa
kujadili mambo mbali mbali.Pia walifundiswa juu ya chimbuko la Siku
ya wanawake Duniani.Somo hilo lilitolewa na mwalimu Dorothy Aidan Mwaluko
katibu tawala mkoa mstaafu.
Mwaluko amewataka wanafunzi hao wahakikishe wanasoma kwa
bidii,na wazingatie yote wanayofundishwa.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa kike,Gradness
Jodocas,alitumia fursa hiyo kumshukru afisa vijana mkoa wa Singida,Frederich
Joseph,kwa uamuzi wake wa kuendeleza program ya malezi na makuzi mema, kwa
vijana katika mkoa wa Singida.
Amemsihi asichoke na badala yake aongeze kasi katika kusimamia
malezi na makuzi kwa vijana,ili kuwa na kizazi chenye hofu ya Mungu.
Kongamano hilo lililofana,pia lilihudhuriwa na afisa michezo
mkoa wa Singida,Amani Mwaipaja,afisa tawala wilaya ya Manyoni Leila
Same,Viongozi wa madhehebu ya dini na walimu kutoka shule shiriki.
Hata hivyo,mkazi wa kijiji cha Ihanja wilaya ya Ikungi,Isekuu
Mwantandu,amewaomba wanafunzi wa kiume wilaya ya Manyoni,wawe wavumilivu
kipindi hiki ambacho jinsia ya kike inapata haki zao kwa mujibu wa sheria
zilizowekwa.Hakuna upendeleo wo wote wanaoupata wanafunzi wa kike.
0 Comments