Ester Chaula Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashaurii ya Wilaya ya Singida Dc akimkabidi fedha kama motisha kwa kina baba,, ikiwa ni mmoja wa baba wa familia aliyeileta watoto wake watatu katika kituo cha Afya cha Ilongero ili wapatiwe chanjo ya Surua Rubella.
Imeelezwa kuwa kampeni ya chanjo ya Surua –Rubelia iliyozinduliwa hivi karibuni sehemu mbalimbali nchini itadhibiti mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Surua uliyoibuka nchini Tanzania katika kipindi cha mwaka 2022-2023.
Kauli hiyo imetolewa na mganga mkuu wa wilaya ya Singida Dkt Grace Charles katika uzinduzi wa chanjo ya Surua –Rubella uliyofanyika katika kituo cha Afya cha ILONGERO.
Dkt Grace amesema kuwa Mkoa wa Singida ulipata jumla ya wagonjwa 345 kati ya mwezi Februari hadi Oktoba 2023 na kati ya hao wagonjwa 6 walitokea Halmashauri ya Singida.
Amesema halmashauri tayari imejiwekea malengo ya kampeni hii kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa matangazo kwenye nyumba za ibada na mikutano na mikusanyiko mbalimbali.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Ester Chaula wakati akimkaribisha mgeni rasmi amewataka wananchi wote kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Aidha Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Mhe Elia Digha ambaye ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya chanjo alisema kuwa chanjo kwa watoto na kina mama ni jambo muhimu kwa kila familia huku akiwataka wakina baba kuhakikisha wanawasindikiza wake zao kliniki ili nao waweze kupata elimu mbalimbali juu ya maswala ya Afya.
Digha ametoa shukrani kwa wajumbe wote waliyofanikisha shughuli hii chini ya kauli mbiu Onyesha upendo mpeleke mwanao akachanje.
0 Comments