DED CHAULA ATOA NAULI KWA KINA BABA KLINIKI.

                                        

              Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Mhe Elia Digha akikata utepe kuashilia uzinduzi wa Chanjo ya kitaifa ya Surua Rubella katika Halmashauri ya wilaya ya Singida .

                      
                             Baba akimshika mwanae ili apatiwe chamjo ya Surua Rubella katika kituo cha Afya Ilongero.

                      

        Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Singida Dc Ester Chaula akiongea kabla ya kukaribisha mgeni rasimi.

                                                                  
                    

Baba akikabidhiwa zawadi ya Fedha tasilim na Mkurugenzi wa Halmshauri ya Singida Ester Chaula kwa kuwaleta watoto wake kliniki kupatiwa chnjo ya Surua-Rubella.

                                         


                Wazazi wa kiume waliyokuja na familia zao kwaajili ya kupatiwa chanjo katika kituo cha Afya Ilongero.


                  

Mratibu wa Chanjo wilaya ya Singida DC Emmanuel Mawi akisoma Rasala katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya chanjo ya Surua Rubella katika kata ya Ilongero.


Mganga Mkuu wa wilaya ya Singida Dkt Grace Charles akitoa taarifa ya maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya chanjo ya Surua Rubella.


Mwenyekiti wa Halmashaur akihakikisha kila mtoto baada ya kupatiwa chanjo hiy anakuwa na wino ikwa ni ishala ya kukamilika kwa zoezi hilo.

Imeelezwa kuwa kampeni ya chanjo ya Surua –Rubelia iliyozinduliwa hivi karibuni sehemu mbalimbali nchini itadhibiti mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Surua uliyoibuka nchini Tanzania katika kipindi cha mwaka 2022-2023.

Kauli hiyo imetolewa na mganga mkuu wa wilaya ya Singida Dkt Grace Charles katika uzinduzi wa chanjo ya Surua –Rubella uliyofanyika katika kituo cha Afya cha ILONGERO.

Dkt Grace amesema kuwa Mkoa wa Singida ulipata jumla ya wagonjwa 345 kati ya mwezi Februari hadi Oktoba 2023 na kati ya hao wagonjwa 6 walitokea Halmashauri ya Singida.

Amesema halmashauri tayari imejiwekea malengo ya kampeni hii kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa matangazo kwenye nyumba za ibada na mikutano na mikusanyiko mbalimbali.

Awali Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Ester Chaula wakati akimkaribisha  mgeni rasmi amewataka wananchi wote kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Aidha Mwenyekiti  wa Halmshauri hiyo Mhe Elia Digha ambaye ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya chanjo alisema kuwa chanjo kwa watoto na  kina mama ni jambo muhimu kwa kila familia huku akiwataka wakina baba kuhakikisha wanawasindikiza wake zao kliniki ili nao waweze kupata elimu mbalimbali juu ya maswala ya Afya.

Digha ametoa shukrani kwa wajumbe  wote waliyofanikisha shughuli hii chini ya kauli mbiu Onyesha upendo mpeleke mwanao akachanje.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments