Na Thomas Kiani
Ikungi
Jumatatu,
11 December, 2023
WATU wawili
wakazi wa kitongoji cha Mwasija Kijiji cha Kintandea kata ya Mtunduru Wilaya ya
Ikungi mkoani Singida Maliki Ramadhani (31) na Shabani Hassani (45) walikutwa
wamekufa kwa kujinyonga kwa kamba siku tofauti wiki iliyopita
nyumbani kwao wanakoishi wakati wake zao hawakuwepo.
Habari
zilizotolewa juzi na mwenyekiti wa kitongoji cha Mwasiya Haji Hamis Nkurwi
amesema katiaka tukio la kwanza Maliki Ramadhani alikutwa amejinyonga kwa
kamba na mama yake baada ya kutomuona nje kwa muda mrefu
jambo ambalo sio kawaida yake huku mlango wa nyumba yake ukiwa umefungwa kwa
ndani akaanza kutia shaka.
Akitoa
maelezo kwa viongozi wa kijiji mama yake Maliki amesema asubuhi
alikwenda Singida mjini na yeye akawafungulia kuku katika nyumba
anayoishi mwanae na baadae akaendelea na shughuli zake.
Katika
maelezo yake mama Maliki alisema mtoto wake aliporudi kutoka mjini alienda
kwake akafunga mlango kwa ndani akafunga kamba juu ya paa la nyumba kwenye
Kenchi Sebuleni akajinyonga akafa.
Habari
zinasema mama yake baada ya kutomuona mwanae nje muda mrefu akatia shaka
akaenda kujua kilichomfanya asitoke, akaita sana lakini hakuitika, akasukuma
mlango akaukuta mgumu umefungwa kwa ndani akaanza kuchungulia kwenye vipenyo
vya mlango akaona miguu ya mwanae imeninginia.
Mama Maliki akijua mwanae amejinyonga,akaanza kulia kwa nguvu akakimbia haraka
kutoa taarifa kwa watu waliokuwepo hapo nyumbani na kwa majirani na kwa
mwenyekiti wa kitongoji Haji Nkurwi na walipofika wakaangalia katika vipenyo nya
mlango wakashuhudia Maliki ameninginia haraka wakatoa taarifa kwa
viongozi wa kijiji
Watu
walipoingia ndani kwa kuuvunja mlango juu ya meza Sebuleni walikuta bahasha na
ndani yake ikiwa na fedha Sh 200,000/= na hazikuwa na maelezo yoyote
wakatoa taarifa hizo Polisi Sepuka wakafika na kushuhudia kifo cha Maliki fedha
hizo wakampa mama yake zitumike kwa mazishi ya mwanae.
Baada
ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa mama yake Maliki na maelezo mengine
kutoka kwa viongozi wa kijiji,Polisi hawakuona shaka juu ya tukio hilo ni
maamuzi yake mwenyewe marehemu, wakatoa ruhusa azikwe kwa taratibu
za dini yake.
Katika
tukio jingine kitongoji hicho hicho siku nne baadae mkazi mmoja wa
eneo hilo Shabani Hassani (45) aligunduliwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba na
mwanae wa miaka 7 saa 4:00 asubuhi wakati akicheza ukumbini na wenzake.
Mwenyekiti
wa kitomgoji hicho Haji Nkurwi amesema mwanae alipoingia ndani ya nyumba ya
baba yake akashtuka kuona baba yake ameninginia, amekufa huku kamba iko
shingoni imefungwajuu kwenye kenchi.
Baada
ya kuona tukio hilo ule mtoto akatoka mbio haraka na akatoa taarifa hizo kwa
watu waliokuwepo hapo nyumbani na wao wakatoa taarifa kwa viongozi wa kijiji na
polisi wa kituo cha Sepuka.
Polisi
wa kituo cha Sepuka walipofika na kushuhudia kujinyonga kwa Shabani na hakuna
ujumbe wowote alioacha kwa familia yake na mkewe hakuwepo kwa muda mrefu yupo
kwao hapakuwepo na shaka juu ya tukio hilo Polisi akaamua azikwe.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Kintandaa Saidi Duyya amethibitisha kuwepo kwa matukio yote
mawili kwenye kitongoji hicho na vyanzo vyake wanahisi ni ugomvi wa ndani kwa
ndani na wake zao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa hakuweza kupatikana kwa simu
yake lakini taarifa anazo za watu hao na imeelezwa ni msongo wa
mawazo kisa cha kujinyomga watu hao.
Mwisho.
0 Comments