IKUNGI YAKUSANYA ZAIDI YA NUSU YA MAPATO TARAJIWA



Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akitoa taarifa ya Mapato ya wilaya hiyo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashari.


Mkuu wa wilaya ya Ikungi Thomas Apson Azipongeza kata zilizofanya vizuri katika ukusanyaji mapato.


SINGIDA

13.11.2023

Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida imekusanya zaidi ya Bilioni 1.5 katika kipindi cha kuanzia mwezi July hadi Nov 2023 sawa na asilimia 59 ambayo ni zaidi ya nusu ya mapato yote wanayolenga kukusanya kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Akisoma taarifa ya ukusanyaji mapato katika kikao cha baraza la madiwani mkurugenzi wa halmashauri hiyo Justice Kijazi amesema kuanzia mwezi july hadi Septemba wamekusanya zaidi ya bilioni 1.1.

Kijazi amesema kati ya fedha hizo mapato huru ni asilimia 46 na mapato fungwa ni asilimia 25 ambapo wanategemea kufikia malengo ya ukusanyaji mapato kwa bajeti kuu ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 2.6.

Aidha mkuu wa wilaya hiyo Thomas Apson amezipongeza kata ambazo zimekusanya mapato huku akiwakumbusha viongozi kuendelea kufanya kazi kiuzalendo kwa manufaa ya jamii zetu na Taifa kwa ujumla.

Nao baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa viti maalumu kata ya Mungaa Helen Petro wamesema hawakubaliani na diwani mwenzao wa kata ya Iseke Leonard Munna sskwa kutokusanya kabisa mapato huku akisema changamoto ni mashine ya kukusanyia yaani POS.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments