AZAM BADO YAIVIMBIA SIMBA TENA NBC PREMER.



 Bado Simba inajiuliza kwanini Azam fc inajiamini sana kwao maana miaka kadhaa iliyopita Azam fc ilikuwa sichochote kwa Simba ilikuwa ikipata ushindi mkubwa bila kipingamizi lakini kwa misimu kadhaa ya hivi karibuni Azam fc imekuwa ikiibuka na ushndi mfululizo.

Mchezo wa leo mashabiki wa Simba wengi wao walijua Azam fc awezi kufua dafu lakini iliwachukua dakika 14 tu za kipindi cha kwanza Prince dube kuandika bao la kuongoza mpaka kipindi cha kwanza kukamilika,

kipindi cha pili Azam fc walikuja na mfumo uleule wa kujilinda zaidi huku wakishambulia kwa kushtukiza tofauti na kawaida yao mbinu hiyo ikiwa na maana ya kumuheshimu mpinzani,iwapo Azam fc wange jaribu kutaka kupishana na Simba mchezo usinge malizika kwa sare kwani Simba walionekana kuwamudu Azam hasa katika eneo la kiungo.

Goli la kusawazisha la Simba lilifungwa na Clatus Chama kutokana na mpira wa adhabu ndogo uliyokwenda moja kwa moja kimiani katika dakika za nyongeza, kwa mantiki hiyo katika msimamo wa ligi Simba itasalia katika nafasi ya 3 huku mtani wao Yanga akiendelea kuongoza ligi.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments