Kituo cha afya kata ya
Msange halmashauri ya wilaya ya Singida kimepokea mashine ya jenereta kutoka
serikalini ili kuwezesha shughuli za matibabu kuendelea pindi inapotokea umeme
kukatika.
Akipokea mashine hiyo
Kaimu Mganga mfawidhi wa kituo hicho Anuari Mchaki ameishukuru serikali kwa
kuwapatia mashine hiyo ambayo itawasaidia sana hasa nyakati za usiku kutokana
na adha waliyokuwa wanaipata.
Dr. Mchaki amesema
mashine hiyo itasaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao walikuwa hatarini
kupoteza maisha kutokana na kukosa huduma muhimu hasa ya upasuaji inapotokea
dharura.
Aidha mwenyekiti wa
halmashauri hiyo na diwani wa Kata ya Msange Eliah Digha ameishukuru serikali
na kueleza kuwa kituo hicho kina upungufu wa vyumba vya kulazia wagonjwa na pia
wanaomba kujengewa jengo la X-ray ili wananchi wapate huduma kwa karibu.
Naye afisa mauzo
kutoka Bohari kuu ya dawa kanda ya Dodoma Omary Mosi akikadhi mashine hiyo
amesema wana jukumu kubwa kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana katika
bohari kuu ya dawa ili waweze kuvihudumia vituo vya afya vya seriakli.
0 Comments