SAUTI YA WARIOBA: “SERIKALI IMETUPA NGUVU KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI”

 

Mkurugenzi wa Mmlaka la maji safi na usafi wa Mazingila SUWASA Sebastian Warioba akiongea na wanahabari.

SINGIDA

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudumu kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi katika Manispaa ya Singida, kutokana na ongezeko la kasi la wakazi katika eneo hilo.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Mkurugenzi wa SUWASA, Sebastian Warioba, amesema upungufu wa maji unaojitokeza kwa sasa unatokana na shughuli za marekebisho na ukarabati wa miundombinu zinazoendelea kwenye baadhi ya maeneo ya vyanzo vya maji.

Amesema kuwa serikali imekuwa bega kwa bega na mamlaka hiyo kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya kuboresha huduma za maji, hatua itakayosaidia kuongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Manispaa hiyo.

Warioba ameongeza kuwa mbali na ukarabati wa miundombinu ya zamani, mamlaka inaendelea kutafuta vyanzo vipya vya maji ili kuhakikisha huduma inapanuka na kukidhi mahitaji ya wananchi wote, hususan maeneo yanayokua kwa kasi.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments