Mwezeshaji kutoka Shirika la Faida Mali Muna Shabani akitoa maelezo mafupi juu ya Semina hiyo ya Siku Mbili.
Vijana kutoka wilaya za Mkalama,Iramba na Ikungi wakipatiwa mafunzo ya uwakala wa pembejeo za Kilimo,
SINGIDA
Na Cales katemana
Katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa
ajira miongoni mwa vijana na kuwazuia kukimbilia mijini au kutegemea ajira za
serikali, Shirika la FAIDA MALI kupitia Mradi wa YEFFA limeendelea kutoa elimu
kwa vijana katika wilaya za Iramba, Mkalama, Ikungi na Singida ili kuwawezesha
kujiajiri kupitia sekta ya kilimo.
Mratibu wa Mradi wa YEFFA, Munna Shabani, amesema mradi huo
unatekelezwa katika mikoa ya Tanga na Singida, ukiwa na lengo la kuwajengea
vijana uwezo wa kuzalisha ajira kupitia kilimo biashara, hususan katika mazao
ya mboga mboga kama vitunguu, nyanya, migomba na mazao mengine ya muda mfupi
yenye tija kubwa kiuchumi.
Ameeleza kuwa mradi huo unalenga vijana wenye umri kati ya
miaka 18 hadi 35, na umekuwa chachu ya kuwainua kiuchumi kwa kuwapa mbinu bora
za kilimo, usimamizi wa masoko, na namna ya kuongeza thamani ya mazao yao.
Aidha, Munna amewataka wauzaji wa pembejeo zaidi ya 200 waliopatiwa mafunzo juu ya ubora wa pembejeo kuhakikisha wanawauzia wakulima pembejeo halisi na bora, pamoja na kuzihifadhi kwa usahihi, ili kuongeza tija katika uzalishaji na kukuza kipato cha vijana wakulima.







0 Comments