MBUNGE WA SINGIDA KASKAZINI APONGEZA WALIMU NA KUWATAKA KUHAMASISHA WANANCHI KUPIGA KURA

 

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini akiongea na waadishi wa habari katika bonanza lililo fanyika kitika viwanja vya Bombadia mjini Singida,

Mwenyekiti wa chama cha waalimu Mkoa Singida Hamis Mtundua akiongea jambo katika bonanza hilo.

Mkuu wa Mkoa waSingida Halima Dendego akikabidhiwa tuzo maaluma na wakurugenzi wa Halmashauri za Manisapaa ya Singida na Singida Dc katibu wa CWT Mkoa na katibu tawala wilaya ya Singida wa kwanza kuli Naima Chondo,


Singida

Na Mwandishi wetu

Mbunge wa Singida Kaskazini, Mhe. Ramadhani Ighongo, amepongeza juhudi za Mkuu wa wilaya Singida Mhe,Godwin Gondwe  wakurugenzi wa Halmashauri za Singida na Manispaa na Chama cha Walimu Mkoa wa Singida (CWT) kwa kuandaa Bonanza la Michezo kwa walimu wa Wilaya ya Singida. Bonanza hili linatarajiwa kuwa jukwaa la kuwakutanisha walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida (Singida DC) na Manispaa ya Singida kwa lengo la kuimarisha mshikamano na kusherehekea mafanikio ya kielimu.

Katika hotuba yake, Mhe. Ighongo alisisitiza umuhimu wa walimu sio tu katika kuimarisha elimu bali pia katika kuwa mabalozi wa mabadiliko ya kijamii. Aliwataka walimu kuhakikisha wanahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi wa serikali ili kuimarisha demokrasia nchini.

"Walimu ni viongozi wa jamii na watu wanaoaminika. Natambua mchango wenu mkubwa si tu katika elimu, bali pia katika kuhakikisha kuwa jamii yetu inakuwa na mwamko wa kidemokrasia. Hakikisheni mnawafikia wananchi na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao," alisema Mhe. Ighongo.

Pia, mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha walimu kuwa jukumu lao linaenda mbali zaidi ya darasani, akiwataka kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika mambo yote ya kijamii.

Bonanza hilo, linalolenga pia kuwapongeza walimu kwa kazi nzuri iliyowezesha Wilaya ya Ikungi kuibuka kinara wa matokeo ya darasa la saba mwaka huu, linatarajiwa kuwa na michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, mpira wa pete, na michezo ya burudani ambayo itajenga afya na mshikamano wa kitaaluma.

 

 

 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments