Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe,Jerry Silaa akiongea na wanachi wa kata ya Tulya alipotembelea katia Ziwa Kitangiri katika ziara yake ya Siku tano mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akiongea na wananchi hao kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mhe,Silaa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida akifurahia Samaki waliyovuliwa kutoka Ziwa Kitangiri akiwamo samaki aina ya Kamongo aliyekabidhiwa mgeni rasimi.
Singida - Iramba
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amemwagiza Mtendaji wa Kata ya Tulya, Wilaya ya Iramba, kuunda vikundi vya wanawake na Vijana wanaojishughulisha na uvuvi katika Ziwa Kitangiri ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kuboresha shughuli zao, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa boti za uvuvi.
Dendego alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa, aliyefika katika ziwa hilo kushuhudia shughuli za uvuvi zinazoendelea.
Akizungumzia hali ya miundombinu, hasa barabara kuu inayoelekea Kata ya Tulya, kupitia Shelui na Tyegelo, Mkuu wa Mkoa aliomba serikali kuendelea na ukarabati wa barabara hiyo ili kufungua fursa za kiuchumi zinazotokana na Ziwa Kitangiri, ikiwemo utalii wa ndani na wa kimataifa.
Kwa upande wake, Waziri Silaa aliwapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, na akaahidi kufikisha salamu na maombi yao kwa mamlaka husika.
0 Comments