Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akitoa taarifa ya maendeleo na Mkoa wa Singida katika maonesho hayo yaliyofanyika kitaifa Mkoa ni Singida.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Comred Martha Malata akitoa salam za cha katika Maonesho hayo.
Mgeni rasmi Waziri wiliam Lukuvi akikagua mabanda katika maonesho hayo
SINGIDA
Maonesho ya saba ya mifuko ya program za uwezeshaji wananchi kiuchumi kanda ya kati yaliyoanza tarehe 8 yamezinduliwa leo mkoani Singida ambapo yataisha tarehe 14 mwezi huu.
Akizindua maonesho hayo yaliyolenga kuwawezesha wananchi
kupata fursa ya kukutana na wajasiriamali na taasisi zingine zinazohudumia
jamii waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, sera bunge na uratibu William Lukuvi
amesema maonesho haya yatatoa fursa nyingi kwa Mkoa wa Singida na kanda ya kati
kwa ujumla.
Amesema wananchi wakiitumia fursa hii vizuri watajikwamua
kiuchumi kwa kujifunza kutoka kwa wenzao ambao wameanza biashara wakiwa na
mitaji midogo waliyowezeshwa au kukopa lakini kwa sasa wanafanya mambo makubwa.
Trilioni 6.8 zimetolewa na program za uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo serikali imeshusha riba katika shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi ili wananchi waweze kumudu na kujiendeleza kiuchumi.
Waziri Lukuvi ametumia nafasi hii kuwaalika wananchi wengine
wa Mikoa ya jirani kufika katika maonesho hayo ili kujipatia na kujionea fursa
hii adhimu kutoka mifuko na sekta za programu za uwezeshaji na sekta zingine za
umma na binafsi.
Awali akizungumza mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego
amesema Mkoa wa Singida umepokea zaidi ya shilingi trilioni 1.9 katika kipindi
cha miaka mitatu kutekeleza shughuli za maendeleo na pia kuweka mazingira
magumu ya serikali kuchachusha uchumu na kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.
Maadhimisho haya yanaongozwa na kauli mbinu isemayo shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unufaike na fursa za uwekezaji.
0 Comments