RC SINGIDA AKUTANA NA VIONGOZI WA MKOA KATIKA KIKAO KAZI.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akisoma taarifa yake ya miezi mitano tangu kufika Mkoa ni hapa. 



Dkt Fatma Mganga akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkarisha mkuu wa Mkoa.





SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amefanya kikao kazi cha tadhimini ya miezi mitano tangu kufika kwake Mkoani hapa, amesema kuwa ameanza kuona mabadiliko ya kiutendaji sambamba na maendeleo ya Mkoa huu.

Hatua hii inakuja miezi michache tangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan afanye babadiliko ya nafasi ya wakuu wa Mikoa ya Iringa Halima Dendego na Petyer Serukamba kubadilisha nafasi hizo za ngazi ya Mikoa.

Dendego amesema anatamani kuona kila kiongozi na mwanachi kwa nafasi yake anafanya kazi kwa bidii na kwa weledi ili kuhakikisha Mkoa na Taifa unapata maendeleo.

Dendego amewataka wajumbe wa mkutano huo kushiriki moja kwa moja katika kuchangia mawazo ya kutatua au kutoa ufafanuzi wa jambo flani litakalo jitokeza katia hoja husuka.

Kikao hicho cha siku tatu kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida kimewakutanisha wakuu wa wilaya za mkoa wa Singida,Wakurugenzi wa Halmashauri wakuu wa Idara ,kamati ya ulinzi ya Mkoa ,makatibu tarafa ,wataalamu mbalimbali kutoka sekta binafsi nasereikalini , Viongozi wa Dini n.k

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments