Naibu katibu (maadili na nidhamu)Tume ya utumishi wa Mahakama Bi Alesia Alex Mbuya akifungua mafinzo hayo mjini Singida.
SINGIDA
27.08.2024
Tume ya
Utumishi wa Mahakama imeweka Mkakati wa kuwafikia wananchi na kutoa elimu
kuhusu uwepo wake, namna inavyotekeleza majukumu yake zikiwemo kamati
zinazopokea malalamiko ya ukiukwaji wa maadili kwa Maafisa wa Mahakama na namna
ya kuwasilisha malalamiko hayo.
Wakiongea
kwa wakati tofauti tofauti washiriki wa mafunzo hayo Maafisa Tarafa kutoka
wilaya na kata mbalimbali Mkoani Singida wamesema kuwa mafunzo hayo
yatakuwa na tija kwani wananchi wamekuwa na uelewa mdogo juu ya kazi za tume
hiyo.
Awali
akifungua semina hiyo Naibu Katibu (Maadili na Nidhamu) Tume ya Utumishi wa
Mahakama ALESIA MBUYA amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kwajengea uwezo
Maafisa hao wa ngazi ya kata ili kuweza kuwaelimisha wananchi juu ya
majukumu ya Tume hiyo.
Mbuya
amesema kuwa viongozi hao ili waweze kwenda kuwaelimisha wananchi kuhusu Tume
hiyo ya Utumishi wa Mahakama ni bora pia wakapatiwa semina ya kujua majukumu
yao na kupewa elimu juu ya maadili ya uongozi.
Aidha
wakati akumkaribisha mgeni rasmi Kaimu afisa habari mkuu kutoka tume ya
utumishi wa Mahakama Lidya Churi amesema kuwa tume ya utimishi imejiwekea
mikakati ya kuhakikisha inatoa elimu kwa wanachi juu ya kuwasilisha malalamiko
yao.
0 Comments