Wafungwa 96 Mkoani
Songwe wamekuwa miongoni mwa wafungwa Zaidi ya 5000 waliopatiwa msamaha wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufuatia maadhimisho
ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika jana jijini Mwanza.
Mapema leo Mkuu wa
Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amefika katika gereza la Mbozi
ambapo wafungwa 45 wanapatiwa msamaha wa Rais huku wafungwa wengine wakiwa
katika Magereza ya Wilaya za Ileje na Songwe ambapo amezungumza na wafungwa hao
kabla hawapewa ruhusa ya kuondoka gerezani hapo.
“Nimeingia gerezani na
kukuta wafungwa waliopata msamaha wa Rais Magufuli wakiwa na furaha na
wamempongeza sana Rais wetu, lakini pia wafungwa waliobaki wamefurahia uamuzi
wa Rais Magufuli wa kutoa msamaha kwani na wao wana tumaini la kupatiwa msamaha
siku za baadae.”, amesema Brig. Jen. Mwangela.
Brig. Jen. Mwangela
ameongeza kuwa wafungwa waliobaki wamempa changamoto mbalimbali zinazowakabili
ikiwa ni pamoja na matatizo ya uhaba wa maji na ucheleweshaji wa nakala za
hukumu mambo ambayo ameahidi kuyashughulikia haraka iwezekanavyo.
Kamishna Msaidizi wa
Magereza Laizack Mfaume Mwaseba amesema amekuwa akipokea malalamiko ya
ucheleweshaji wa nakala za hukumu kutoka kwa wafungwa na amekuwa akiwasiliana
na mahakimu ili waweze kuzitoa nakala hizo kwakuwa ucheleweshaji huo unawanyima
haki wafungwa ya kukata rufaa.
Ameongeza kuwa pamoja
na changamoto ya maji katika gereza hilo kuna changamaoto za uhaba wa vitendea
kazi na sare kwa wafungwa mambo ambayo tayari wamesha yawasilisha kwa kamishana
Mkuu wa Magereza kwa ajili ya utatuzi.
Mmoja wa wafungwa wa
gereza la Mbozi Victoria Adam amemshukuru Rais Magufuli kwa msamaha alio mpatia
na kumuombea kwa Mungu aendelee kumlinda huku akieleza kuwa amejifunza mambo
mengi alipokuwa gerezani na sasa anaenda kuwa raia mwema.
Naye Fred Andrea Daud
ambaye amepata msamaha wa Rais Maguufuli amesema bahati aliyoipata ya Msamaha
ataitumia vizuri kwa kufanya kazi halali kwakuwa Vijana wengi wamekuwa
wakichagua kazi ambazo zinawaingiza katika matatizo
Ameongeza kuwa
magereza ni sehemu ya urekebishaji na yeye amerekebika hivyo anawashauri vijana
wote wafanye kazi halali ambazo hazitawaletea matataizo kwakuwa kazi halali
zipo nyingi.
Mapema leo Mkuu wa
Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akiwa katika gereza la Mbozi
ambapo wafungwa 96 Mkoani Songwe wamepatiwa Msamaha wa Rais wa Jamhuri wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho
ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania
Wafungwa
waliopatiwa Msamaha wa Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania
wakiwa nje ya gereza la Mbozi kwa ajili ya kuondoka, Jumla ya wafungwa 96
Mkoani Songwe wamepata msamaha wa Rais Magufuli.
Wafungwa
waliopatiwa Msamaha wa Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania
wakiondoka katika gereza la Mbozi; Jumla ya waafungwa 96 Mkoani Songwe wamepata
msamaha wa Rais Magufuli.



0 Comments