NAIBU Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Bwana Eliasi Kwandwikwa amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni inayojenga Kituo cha Ukaguzi wa pamoja cha wilayani Manyoni,Impresa di Costraction Ing. Montovani ya Nchini Italia kuhakikisha anamaliza kazi ya ujenzi wa kituo hicho ifikapo sept,09,2018 ili kuiepushia serikali hasara zisizokuwa za lazima.
Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo katika Kijiji cha Muhalala,Wilayani Manyoni,Mkoani Singida wakati alipotembelea na kukagua shughuli zinazoendelea katika mradi wa Kituo cha ukaguzi wa pamoja na kuongeza kwamba kuwa na mradi ni jambo moja na kuukamilisha kwa wakati ni jambo jingine.
Hata hivyo Bwana Kwandikwa amefafanua kwamba ni matarajio ya serikali kwamba ifikapo mwishoni mwa mwezi wa tisa,mwaka huu mradi huo utakuwa umefikia mwisho kama ilivyo kwenye mkataba na kama hautamalizika kwa muda wa mkataba, hategemei kuwepo gharama zitakazoongezeka kwa upande wa serikali kwani endapo itatokea hivyo itakuwa ni hasara kwa serikali,jambo ambalo hategemei kutokea.
Kwa mujibu wa Kwandikwa ametumia pia fursa hiyo kumshauri Mkandarasi wa ujenzi huo wa Kituo cha ukaguzi licha ya kufanya kazi nzuri,lakini alimtahadharisha kutobweteka na sifa hiyo aliyopewa na badala yake alimtaka kuongeza kasi zaidi ili kazi iweze kufikia mwisho katika kipindi cha mkataba.
Hata hivyo Naibu waziri huyo mwenye dhamana ya kusimamia wizara ta Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ameweka bayana changamoto ya madereva walevi wanaotumia vyombo vya moto,kwa hali hiyo kituo hicho kitatumika kuwakagua madereva wanaotumia barabara hiyo ili kuwabaini wale wanaokunywa pombe nyakati za asubuhi na wanapoendesha vyombo vya moto.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo ameweka bayana kwamba ili kukabiliana na madereva walevi na wazembe,wakati umefika kwa serikali kuanzisha maabara ndogo kwenye barabara ili kuwafanyia uchunguzi madereva,na endapo watabainika,watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Singida,Mhandisi Leonard Kapongo ameahidi kuwasimamia Mkandarasi pamoja na Mhandisi mshauri ili waweze kufanyakazi na wahakikishe kwamba kazi zote zilizopangwa kwenye Mkataba huo zinakamilika kwa muda uliopangwa katika mkataba na kuhakikisha hapatakuwa na gharama za ziada zitakazotokana aidha kwa uzembe wa Mkandarasi au uzembe wa Mhandisi mshauri.
Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa mradi,Mhandisi Patrick Marko amemhakikishia Naibu Waziri huyo kwamba baada ya vifaa vya ujenzi wa mradi huo kuwasili kutoka Nchini Uturuki,wanatrajia kufanya majaribio juni,mosi,mwaka huu,
MRADI wa Vituo vikuu vya ukaguzi wa pamoja unafadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya kwa gharama za EURO 9,537,609.90 bila VAT na muda wa ujenzi wa mradi huo ni miezi 18.
0 Comments