Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira
Suwasa mkoani Singida inajumla ya wateja wa maji 10,720 katika manispaa ya
Singida ambao kati yao wateja walio hai ni 8,466.
Takwimu hizo zimetolewa na mkurugenzi wa mamlaka
hiyo Mhandis,Patrick Nzamba wakatia akitoa maelezo mafupi katika siku ya
maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana tarehe 16 mwezi March na inataria
kufikia kilelen march,22 mwaka huu.
Mhandis Nzamba amesema wanaendelea kuhamasisha
wananchi kujitokeza ilikuunganishiwa maji huku akitoa wito kwa wateja wote
kuzingatia kulipa Ankara za maji kwa muda muafaka.
Aidha amewaomba wateja wenyemita kuwa waaminifu
kwa kutokwepesha maji yasipite kwenye mina ta kuongeza kuwa hatua kali
zitachukuliwa kwa yeyote atakaye baini kufanya kosa hilo.




0 Comments