MILION 20 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 16 MKOANI HANANG

HALMASHAURI ya Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara imekabidhi vikundi 16 vya wanawake,vijana pamoja na walemavu hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni ishirini ili viweze kukuza mitaji,kuboresha maisha na kuongeza uzalishaji kwenye baadhi ya viwanda vidogo walivyoanzisha.

Akikabidhi hundi hiyo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,George Bajuta alisema vikundi hivyo vimefanikiwa kupata fedha hizo baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa kati ya vikundi zaidi ya 1,000 vilivyopo katika wilaya hiyo.

Hata hivyo Bajuta hakusita kuvisisitiza vikundi hivyo kuhusu umuhimu wa kurejesha fedha hizo walizokopeshwa kwani utaratibu huo ni wa mzunguko ili na vikundi vingine navyo viwezo kunufaika na mpango huo.

Naye Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Doris Nhomange alivitaja vikundi vya wananwake vilivyonufaika na mikopo hiyo na kata zikiwa kwenye mabano kuwa ni pamoja na Kikundi cha Amani(Simbay),Tegemeo(Kateshi),Juhudi(Nangwa),Amani(Dawali),Waida (Mogitu),Kumekucha (Garawa),Kilimo (Endasiwold),Uvumilivu (Dumbeta),Uyanjo (Getanuwasi na Semeni(Measkroni).

Kwa upande wa vikundi vya vijana ni Eforti kutoka Kateshi,Daraja Production kutoka Darajani Jorodomu,Kikundi cha walemavu Ambianse kutoka Ganana,Ambianse kutoka Ganana,Vijana na kazi kutoka Basotughani na Mkombozi kutoka Basotughani
Mwenyekiti wa Umoja wa mafundi Kateshi,Mohamedi Yusufu Mashaka pamoja na kuishukuru Halmashauri kwa mikopo hiyo,lakini hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha vijana wa wilaya ya Hanang kuunda vikundi,wavisajili na kisha ndipo waombe mikopo.
   
Katika hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu aliweka bayana kuwa katika mkutano wa Lac Dodoma na katika kikao hicho ilibainika kwamba Hanang ilikuwa ikidaiwa zaidi ya shilingi milioni mia tatu walizokuwa wamelimbikiza utoaji huo wa mikopo ya wananwake na vijana.

“Sasa leo mnatoa shilingi milioni ishirini tunaomba tujue hizo zilizobaki zinatolewa lini watu wanataka kuwa na mitaji jamani ili muweze kupata kodi zaidi na ushuru zaidi.”alihoji Dk Nagu.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo suala hilo liliongelewa kwa umuhimu mkubwa na kwamba wajumbe wa mkutano huo waliazimia fedha hizo zitolewe katika kipindi kisichozidi miezi miwili na kuomba kupatiwa majibu ni lini fedha hizo zitapatikana ili wananchi waweze kunufaika nazo.

Akijibu hoja ya Mbunge Dk.Mary Nagu,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,George Bajuta licha ya kutokanusha hoja hiyo lakini alijibu kwamba  waliohusika kula fedha hizo ambao hata mbunge huyo anawajua mpaka sasa bado hawajawarudishia.

“Unajua aliyetafuna ni nani,aliyelimbikiza ni nani na hawatajaturudishia mpaka leo na hata Tanzania bado inadaiwa na hawajalipa madeni yao sisi tunaanzia pale tuliposhikilia tunakwenda mbele,tusiangalie nyuma utageuka kuwa jiwe,na hata wabunge wahoji namna gani mkono unajikuna pale unapoishia”alisisitiza Mwenyekiti wa Halmashauri.


Ni Baadhi ya vikundi vilivyopatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni ishirini na kuhimizwa juu ya kurejesha mikopo hiyo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa ili vikundi vingine navyo viweze kupatiwa mikopo hiyo.

Ni Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Hanang,Doris Nhomange(wa kwanza kulia) akizungumza na vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo na kuwashauri kwamba wakazitumie fedha hizo kwa madhumuni waliyoombea.

Ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,George Bajuta (wa pili kutoka kulia) akiongoza mkutano wa kawaida wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Hanang,uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
 Ni Mkuu wa wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Sara Msafiri akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Hanang na kusisitiza juu ya umuhimu wa kuhifadhi misitu pamoja na kuvilinda vyanzo vya maji kwenye maeneo yao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments