VIA SKY
NEWS
Rais wa
Urusi Vladimir Putin ameibuka mshindi kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine
ujao wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa. Hata kabla ya kura zote
kuhesabiwa tayatri alikuwa amejizolea asilimia 76 kwa mjibu wa tume ya
uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa
kutangazwa mshindi amsema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio
aliyoyafikia katika uongozi wake.
Putin ameongeza kuwa hii ni
uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na kwamba hana mpango wowote wa kufanya
marekebisho ya katiba na kusisitiza umoja na mshikamano.
"Hadi hapa sina mpango
wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya katiba,kuhusiana na unyekiti na
serikali kwa ujumla.Nilikwisha sema awali kwamba nafikiria suala hilo.Lakini
kuanzia leo naanza kufikiria kwa undani,kwa sababu nilipaswa kusubiria matokeo
ya uchaguzi kwanza.Mabadiliko yote yatatangazwa yakifuatiwa na uzinduzi.."
Akijibu maswali kutoka kwa
waandishi wa habari Putin amekwepa swali alilotakiwa kueleza kama atagombea
katika muhula ujao pia.
"Kwangu kile mnachotaka
kuniuliza inakuwa kama mizaha Fulani hivi,hebu tuhesabu,ina maana nitasalia
madarakani hadi nikiwa na miaka 100? Hapana hapana hapana. "
Ushindi huu mkubwa ambao
ulitarajiwa,umekuwa na ongezeko la kura ikilinganishwa na ushindi wa asilimia
64 mwaka 2012.Ambapo m,pinzani wa karibu wa Putin milionea Pavel Grudinin,yeye
alipata asimilia 12.




0 Comments