TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
(PRESS RELEASE)
MAUAJI
19.03.2018
Mnamo tarehe
08.09.2010 Huko katika Kituo cha Polisi Kinampanda, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa
Singida Benard Shumba, (47), Mnyiramba,
Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Yulansoni, Kata na Tarafa ya Kinyangiri,
Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida alifika Kituoni hapo na kutoa taarifa kuwa
Mke wake aitwaye Tabu Robert, (28), Mkazi waYulansoni haonikani nyumbani kwake.
Juhudi za kumtafuta kwa kushirikiana na ndugu zake zilianza bila mafanikio
ndipo alipoendelea kuishi kijijini hapo akitunza mwanae aliyeachwa na Mama
yake.
Jeshi la Polisi
kwa kushirikiana na Raia wema liliendelea kumtafuta bila mafanikio ambapo siku
ya tarehe 17.03.2018 lilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa Tabu Robert
hakupotea bali aliuwa na Mme wake. Askari wa Jeshi la Polisi walifika nyumbani
kwa Mtuhumiwa na kufanikiwa kumkamata
ambapo alihojiwa na kukiri kufanya mauaji hayo siku ya tarehe 07.09.2010 majira
ya saa 2:00 usiku akiwa nyumbani kwake na kukiri kuwa baada ya kutenda kosa hilo
aliuchukua mwili wa Marehemu na kwenda kuuficha kwenye mti wa mbuyu ambao una
shimo kubwa na kisha kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi hicho.
Uchunguzi wa
Polisi umebaini kuwa chanzo cha mauaji
hayo ni ulevi wa pombe za kienyeji wa Marehemu
na kumuacha Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka miwili peke yake kitendo
ambacho kimekuwa kero kwa Mtuhumiwa.
Siku ya tarehe 18.03.2018 majira ya saa 10:00 jioni
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi walifika eneo la tukio ambalo lipo
umbali wa Mita 600 kutoka nyumbani kwa Mtuhumiwa na kukuta masalia ya mifupa, fuvu na mbavu
zidhaniwazo kuwa ni za binadamu ndipo Polisi walipochuka sampuli za mabaki hayo
kwa uchunguzi zaidi na mabaki mengine kukabidhiwa kwa Ndugu wa Marehemu kwa hatua za mzishi.
Kuhusiana na tukio hilo Jeshi la Polisi
linamshikilia mtuhumiwa Benard s/o Shumba kwa uchunguzi zaidi na baada ya
uchunguzi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kutoa Wito
kwa wananchi wote kuendelea kutoa Taarifa zitakazosaidia kuwabaini wahalifu
katika maeneo yao ili kuzidi kutokomeza uhalifu Mkoani Singida pia kuacha
tabia za kujichukulia sheria mkononi pindi wanapokuwa na migogoro ya aina
yoyote bali watoe taarifa kwa viongozi wa Serikali za Mitaa au katika vituo vya
Polisi vilivyokaribu na wao ili matatizo yao yatatuliwe kisheria.
.










0 Comments