PICHA ZA MATUKIO YA TAMASHA LA MWANAMKE WA NGUVU KATIKA VIWANJA VYA UKUMBI WA UHASIBU SINGIDA

Mkurugenzi wa Standard Fm Mr James Daudi (kulia) akibalishana mawazo na  katibu wa mkuu wa mkoa  kabla ya kuingia ukumbini.

Bw Jamse Daudi Mkurugenzi wa Standard Fm akitoa ufafanuzi juu ya upanuzi wa masafa ya Radio kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi wakati wa kukakua mabanda kabla ya kuingia ukumbini.


Mkurugenzi wa kituo cha Radio Standard Fm Singida Bw James Daudi akimkaribisha mgeni rasimi mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi katika  kongamano la MWANAMKE WA NGUVU lillilo ratibiwa na radio hiyo .
Stella Ngenje mtangazaji wa kipindi cha zinduka akiongea juu ya wasifu wa mwanamke mbele ya mgeni rasimi mkuu wa mkoa wa Singida .
Mgeni rasimi mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akiongea na wakina mama waliyoudhulia  katika kongamano hilo.


Mama mjasiliamali akielezea namna anavyojishugulisha na shuguli za ujasiliamali na kupata mafanikio kupitia vikundi  mbalimbali vya vicoba.


Mratibu kutoka VICONET Bi Happy Francis akikabidhiwa miche ya mikorosho iliyotolewa na mkuu wa mkoa .


Picha ya pamoja na staff ya Radio Standard Fm 90.1 Singida Mkurugenzi na mkuu wa mkoa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida .
Dr Rehema Nchimbi akiondoka katika viwanja hivyo vya Uhasibu baada ya kuongea na kinamama  huku akitoa  wito  kupanda mikorosho na kukabidhi miche ya mikorosho.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba 
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Singida Debora Magiligimba, amewataka wanawake kutoa taarifa za vitendo vya  ukatili vinavyofanywa na baadhi, ya wanaume katika familia.

Magiligimba ameyasema hayo leo mchana wakati akitoa salaam katika tamasha la mwanamke wa  nguvu, lililoandaliwa na Standard Radio na kufanyika  katika ukumbi wa chuo cha TIA Singida.

Amesema kwa wanawake kutoa taarifa katika dawati la jinsia na watoto dhidi ya  vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ,kutapunguza vitendo hivyo.


Kwa upande mwingine Kamanda Magiligimba ametumia Fursa hiyo kuwataka wanaume kutofanya vitendo hivyo, badala yake waelekeze nguvu zao katika shughuli za kuinua kipato kwa familia.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments