|
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Bw Miraji Mtaturu akifungua mafunzo . |
Wanawake wamekuwa hawana ujasili wa kutoa taarifa juu ya ukatili wanaofanyiwa kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa wanaume wao.
Hayo yamezungumzwa na afisa maendeleo wilayani Ikungi Mkoani Singida Bi.Kuluthumu Sasya katika uzinduzi wa utetezi dhidi ya mila potofu kama ukeketaji wa wanawake na udhalilishaji wa kijinsia wilayani humo.
Bi.Evaline Lyimo ni mratibu wa shirika la Save The mother and children Tanzania amesema kuwa mradi huo unatarajia kuwafikia watu 3600 ikiwemo kutoa mikutano katika vijiji mbalimbali wilayani Ikungi mkoani Singida.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ikungi Bw.Miraji Mtaturu amesema kuwa mradi huo utasaidia jamii katika masuala mazima ya ukeketaji kwa wanawake na uzalilishaji wa kijinsia .
|
Bi Evalin senge Lyimo ni mkurugenzi mtendaji wa Save The mother and children Tanzania akisoma risala fupi mbelele ya mkuu wa wilaya Ikungi Bw Miraji mtatulu (kulia). |
|
Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Ikungi Bi Kuluthumu Sasya akifafanua juu ya njia mpya ya kukeketa kwasili watoto wakiwa bando wachanga na namna wanavyo piga vita tabia hiyo |
|
Ngaliba kutoka wilaya ya Ikungi wakielezea jinsi walivyo kuwa wakifanya ukeketaji kwa watoto wakike baada ya kupata elimu juu ya athali ya keketaji waliamua kuacha tabia hiyo. |
|
Kikundi cha ngoma cha LITI kutoka wilaya ya Ikungi |
Tuandikie Maoni Yako Hapa
0 Comments