Diwani wa kata ya Unyanga Bw Geofrey Mdama akiongea katika mahafali hayo |
Shule ya msingi Unyianga iliopo katika Halmashairi
ya Manipaa ya Singida inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo matundu ya
vyoo ,madawati,vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika mahafali
ya 56 ya darasa la Saba Bw.John Abel amesema kuwa shule hiyo kwa upande wa
miundo mbinu ina mahitaji mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu pamoja na
nyumba za walimu.
Akijibu risala hiyo mgeni rasmi ambaye ni diwani wa
kata ya Unyianga Bw.Geofrey Mdama amesema kuwa atahakikisha suala la upungufu
wa madawati linakamilika ikiwa ni pamoja na kutoa mchango wake kwa ajili ya
chakula cha mchana shuleni.
Darasa la saba wanatarajia kufanya mtihani wao wa
kuhitimu shule ya msingi mnamo septemba ,6,mwaka huu huku wakitakiwa kufanya
vizuri katika masomo yako na kuongeza kiwango cha ufaulu.
0 Comments