Kaimu mshauri wa jeshi la akiba mkoa wa Singida Capten M.W Matyeni akichangia damu katika maadhimisho hayo ya JWTZ. |
Wanajeshi wa akiba wakipata maelekezo baada ya kuchangia damu pia. |
Mifuko 50 ya damu salama imepatika katika zoezi hilo. |
Cales katemana nikichangia damu pili baada ya kuona kilo zangu zimefika 120 nikaona sinabudi kutoa damu . |
SINGIDA
Katika kuadhimisha miaka 53 Ya kuanzishwa kwa jeshi la ulinzi na usalama la Tanzania JWTZ mkoani singida wanajeshi wamefanya usafi maeneo mablimabli ikiwemo kata ya mwankoko na uchangiaji wa damu salama
Katika kuadhimisha miaka 53 Ya kuanzishwa kwa jeshi la ulinzi na usalama la Tanzania JWTZ mkoani singida wanajeshi wamefanya usafi maeneo mablimabli ikiwemo kata ya mwankoko na uchangiaji wa damu salama
Akizungumza na Standard fm wakati wa utoaji damu kaimu
mshauri wa jeshi la akiba mkoa wa singida Capten
M.W Matyeni amefafanua juu ya zoezi zima la wiki ya kumbukumbu ya
kuanzishwa kwa jeshi hilo.
Aidha ametoa wito kwa vijana kujiunga na jeshi la mgambo ili
kuweza kuwa na uzalendo pamojan kutetea nchi yao.
Kwa upande wa mratibu wa damu salama mkoa wa Singida Bw Osca
msenga amewapongeza wanajeshi kwa kujitolea damu katika kuadhimisha siku hiyo.
Huko wilayani mkalama mkuu wa wilaya ya hiyo Jackson Masaka ameliagiza Jeshi la Mgambo wilayani hapo
kuwakamata wananchi ambao Mazingira yao ni Machafu.
Mhandisi Masaka ametoa agizo hilo wakati akizungumza na
wanamgambo katika Maadhimisho ya Siku ya Majeshi yaliyofanyika katika Ofisi ya
Kijiji cha Nguguti.
Aidha katika Maadhimisho hayo Askari hao wa Jeshi la Mgambo
wamefanya usafi katika Zahanati ya Nguguti ambapo Mhandisi Masaka amewataka
kushiriki zaidi katika shughuli za kijamii ili kuonyesha uzalendo wao.
0 Comments