Shekh Issa Nassor katika swala ya Eid manispaa ya Singida viwanja vya s/m Ukombozi |
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) meshauriwa kuelekeza nguvu zake kwenye madhehebu ya dini, kwa kile kilichotajwa kuwa baadhi ya taasisi zake zimejaa ufisadi na dhuluma
Sekhe wa taasisi ya Thamaratul Kadiria mkoani
Singida,Issa Nassoro ametoa wito huo wakati akitoa mawaidha kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku kuu ya Eid el Haji yaliyofanyika kwenye kiwanja cha shule
ya msingi Ukombozi mjini Singida
Amesema baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini
ambao wengi hawapendani wao kwa wao, wamekuwa wakiuza viwanja na mali mbali
mbali ya madhehebu na taasisi zao, na kujinufaisha binafsi.
Sheikh Nassoro ametumia fursa hiyo kuiomba TAKUKURU kuelekeza macho yao kwenye
madhehebu na dini na taasisi zake,ili kukomesha vitendo hivyo ambayo havikubakili
kijamii na Mungu pia havipendi.
Katika hatua nyingine,Sheikh Nassoro,amesema
vitendo hivyo vyote vinafanywa na binadamu ambao hawana hofu ya Mungu.
0 Comments