Kaimu katibu tawala wilaya ya Singida Bw Fute akiongea katika uzinduzihuo katika ukumbi wa RC MISION Singida mjini |
Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo AMDT yenye
makao makuu yake jijini Arusha imezindua mradi wake mkoani Singida ikiwa na
lengo kukuza na kuenedeleza kipato kwa
wakulima hususani wa Alizeti.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Singida,katibu
tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoa wa Singida Stansilausi
Choaji amlishukuru shirika hilo kwani ni fursa kwa mkoa wa Singida.
Akisoma Risala mbele ya mgeni Rasmi mkurugenzi wa shirika la
Faida mali mkoani Singida Bw.Tom Silayo amesema wamekuwa wakitoa mafunzo katika
makundi mbalimbali ya wakulima ikiwemo kilimo biashara.
Mwenyekiti wa ushirika wa wakulima wa alizeti Tanzania
Bw.Peter Helly amesema mradi wa AMDT utasaidia kutatua changamoto za wakulima
0 Comments