Dr Nchimbi akizungumza na wanahabari leo |
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dr: John Pombe Joseph
Magufuli , hapo kesho anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja mkoani Singida
,kufungua rasmi barabara ya kiwango cha lami ya Manyoni – Itigi hadi chaya
mpakani na mkoa wa Tabora.
Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Singida,Dr:Rehema wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo.
Dk.Nchimbi amesema kuwa
uzinduzi huo wa barabara yenye urefu wa kilometa 89.3, unatarajiwa kufanyika
kuanzia majira ya saa tatu asubuhi kwenye mzunguko au Round about ya barabara katikia
mji mdogo Itigi wilaya ya Manyoni.
Amesema tukio hilo ni muhimu kwa kila mwenye nafasi kuhudhuria,na
kwamba barabara hiyo itachochea ukuaji wa uchumi kwa mikoa ya kanda ya
kati.
0 Comments