Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr:John Pombe Magufuli ametumia siku ya kumbukumbu ya mashujaa kufungua rasmi barabara ya Manyoni – Itigi-Chaya
ya kiwango cha lami yenye
urefu wa kilomita themani na tisa nukta
tatu.
Akizungumza
wakati wa Uzinduzi huo ambao umefanyika katika
halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni Rais Magufuli
amewataka watanzania kukumbuka walikotoka kwani kwa kipindi kifupi Barabara nyingi hapa nchini
hazikuwa na Lami.
Amesema
uwepo wa barabara hizo umepelekea kupatikana kwa mawasiliano mazuri na
kukuza uchumi wa wananchi.
Aidha Rais Magufuli amewataka wananchi kufanya
kazi na kuwaomba wakuu wa mikoa, wilaya na wenyeviti wa mitaa kuwasihi wananchi
kufanya kazi kwani serikali haitatoa chakula pale njaa itakapo tokea kitika
mkoa au wilaya husika.
Awali mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi amemshukuru mheshimiwa rais kwa ujenzi wa barabara hiyo na kumuhakikishia kuitumia kwa
kuwa hamashisha wananchi kujiletea maendeleo na kubadili maisha yao.
1. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua
barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 mapema leo, kulia
kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa na
kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi.
2. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
wakazi wa Itigi mara baada ya kuzungumza nao na kuzindua barabara
Manyoni-Itigi-Chaya, ambapo pamoja na mambo mengine ameagiza ujenzi wa barabara
ya Chaya-Nyaua yenye kilomita 85 na ujenzi uanze ndani ya siku 45 ili barabara
hiyo ikamilike kwa kiwango cha lami.
0 Comments