CHAMA cha mpira wa miguu
mkoa wa Singida (SIREFA),kinatarajia kufanya uchaguzi mdogo kuziba mapengo
jumamosi mei 20 mwaka huu.
Uchaguzi huo
unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka mkoani Singida,unatarajiwa
kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano chuo cha maendeleo ya wananchi (FDC),mjini
hapa.Na utaanza saa tatu asubuhi.
Nafasi zinazongombewa ni
pamoja na nafasi ya mwenyekiti iliyoombwa na Hussein Zuberi Mwamba,Samweli
Nakei,Erasto Sima,Mussa Ramadhani Sima na Iddi Mnyampanda.
Nafasi ya makamu
mwenyekiti,imeombwa na Ally Ramadhan Nkhangaa pekee,wakati nafasi ya mweka
hazina msaidizi, imeombwa na mgombea pekee Hamza Mussa Ntoga.
Nafasi ya katibu mkuu
imeombwa na Rashidi Mohammed Komba na Edward Ihonde.Nafasi ya mjumbe mkutano
mkuu TFF,imeombwa na Manase Abel na Nufus Ndee.
Uchaguzi huo
mdogo,unafanyika baada ya viongozi waliochaguliwa mwishoni mwa mwaka jana
kwenye nafasi hizo, kujiuzulu kutokana na sababu mbalimbali,ikiwemo sifa ya
elimu.
Akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake jana,mwakilishi wa vilabu SIREFA,Gabriel Gunda,alisema
maandalizi yote muhimu yanaendelea vizuri na yatatarajiwa kukamilika kwa wakati.
Gunda alisema kuwa
mkutano huo mdogo wa uchaguzi ambao alitarajiwa waziri wa mambo ya ndani
Mwagullu Nchemba kuwa mgeni rasmi,hatafika kutokana na sababu zisizozuilika.
“Kwa hiyo sasa mkuu wa
mkoa Dk.Rehema Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Tunatarajia pia mjumbe
kutoka kamati ya uchaguzi TFF atakuwepo”,alisema.
Alisema wapiga kura
katika uchaguzi huo,ni mwenyekiti,katibu na mjumbe wa mkutano mkuu SIREFA
kutoka wilaya zote za mkoa wa Singida.
“Pia atakuwepo
mwakilishi wa vilabu kutoka wilaya zote sita.Vile vile wajumbe kutoka vyama vya
TAFCA na FRAT ambao vitawakilishwa na mwenyekiti na katibu”,alisema Gunda.
0 Comments