Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo akiongea na wakazi wa kata ya Mandewa manispaa ya Singida.
|
Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyampimbile akisisitaza juu ya usafi wa mazingila
|
Wananchi
wametakiwa kutunza amani ya nchi iliyopo pamoja na kuulinda muungano ili
kudumisha ndoto ya waasisi wa taifa hili.
Akiongea wakati wa maadhimisho
ya Siku ya muungano ambayo imeambatana na zoezi zima la usafi mkuu wa wilaya ya
Singida Bw, Elias John Tarmo amesema muungano unapaswa kulindwa.
Amesema waasisi wa muungano
walikuwa na dhamira ya kweli ya kuhakikisha taifa linakuwa na nguvu za
kujilinda pamoja na nguvu za kiunchumi
Bw, Tarmo ameongeza kuwa miaka ya 1960
viongozi hao na wengine wa afrika kama Kwame Nkuruma kutoka Ghana walikuwa na kusudio la kuunga muungano wa
afrika.
Kwa upandea wake mkurugenzi wa
halmashauri ya manispaa ya Singida Bw, Bravo Kizito amesema wameamua
kuadhimisha sikuku ya muungano kwa kufanya usafi kwani huwezi kusherehekea
hukua mazingira yakiwa machafu.
0 Comments