Kesi inayombakiri aliyekuwa mfanyakazi wa Bank ya Posta tawi
la Singida Elihuruma Emmanuel imeendelea kusikilizwa katika makahama ya wilaya
ya Singida kwa mashahidi wawili kutoa ushahidi wao.
Shahidi wa kumi Damiano Nkumbo (45) ambaye alitakiwa na
wakili wa serikali Bi.Petrida Muta kuiambia mahakama siku ya tukio ilivyokuwa
amesema mshitakiwa alianza kutoa semina kwa wanavikundi mbalimbali katika
vikundi.
Aidha Bw.Nkumbo ameieleza mahakama kuwa mshitakiwa aliwasihi
kufungua Akaunti ili waweza kupata mkopo kwa urahisi ambapo walitii wito huo.
Shahidi wa kumi na moja amesema kuwa baada ya kufungua
akaunti kama wana kikundi cha Nguvu kazi walikusanya shilingi laki tatu kwa
ajili ya dhamana ya mkopo ambapo waliwasiliana na mshitakiwa na hatimaye kukutana
eneo la kibaoni na kumkabidhi hiyo fedha.
Hata hivyo Hakimu wa mahakama hiyo Bi.Joyce Minde
ameahirisha kesi hiyo hadi April,13 mwaka huu itakapo kuja kwa ajili ya
kuendelea kisikilizwa kwa mashahidi wawili waliobaki.
0 Comments