Makongoro Nyerere |
Chama cha
Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina ya wanachama wake 12 walioteuliwa kugombea
ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kwenye
mkutano wa Bunge ujao.
Akisoma
majina hayo leo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa wameteua wananchama hao miongoni
mwa wengi zaidi ya 400 waliokuwa wamechukua fomu kugombea nafasi hizo.
Mchanganuo
Miongoni
mwa wabunge 9 watakaokwenda Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha Tanzania, 6
watatoka CCM. Kufuatia idadi, hiyo CCM imesema kuwa itatoa wabunge watatu wa
kiume na watatu wa kike ambapo miongoni mwao wanne watatokea Tanzania Bara na
wawili watatokea Tanzania Visiwani.
Walioteuliwa
kugombea nafasi hizo ni;
Wanawake
Tanzania Bara;
1
Zainabu Rashid Mafaume Kawawa
2
Happiness Elias Lugiko
3
Fancy Haji Nkuhi
4
Happiness Ngoti Mgalula
Wanaume
Tanzania Bara;
1
Dkt Ngwaru Jumanne Maghembe
2
Adam Omari Kimbisa
3
Anamringi Issay Macha
4
Charles Makongoro Nyerere
Wanawake
Zanzibar;
1
Maryam Ussi Yahya
2
Rabia Abdallah Hamid
Wanaume
Zanzibar;
1
Abdallah Hasnu Makame
2
Mohammed Yussuf Nuh
Miongoni wa wagombea hawa 12, Bunge litapiga kura kuchagua
wabunge sita watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki kwa
tiketi ya CCM.
0 Comments