Mkuu wa Mkoa wa Singida akiwa katika kiwanda cha Mafuta cha Mount Meru manispaa ya Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akiwa katika kiwanda cha Singida Fres ikiwa ni ziara ya kutembelea viwanda vya Manispaa ya Singida.
SINGIDA
Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Halima Dendego, amewapongeza wawekezaji wa ndani hasa katika sekta ya viwanda
vya mafuta ya kupikia, Mount Meru Mellers LTD, Singida Fresh Oil Mill na
kiwanda cha Pamba cha Biosustain vilivyopo mkoani Singida akisema uwepo wa
uwekezaji huo unaipunguzia Serikali mzigo wa kuagiza mafuta ya kupikia kutoka
nje na kuleta ajira kwa vijana.
RC
Dendego, ametoa pongezi hizo katika ziara yake ya kutembelea viwanda katika
halmashauri ya Manispaa ya Singida ambapo amesema, uwekezaji katika viwanda vya
mafuta utasaidia serikali katika kutimiza lengo lake la kuzalisha mafuta ndani
ya nchi.
Akizungumzia
kiwanda cha Singida Fresh Oil Mill, Dendego amekiri kupokea taarifa ya kuwa
asilimia 95 ya ukamilishaji mradi huo tayari umefikiwa na zaidi ya watu 200
wanatarajiwa watapata ajira, hii ni kuunga mkono serikali katika juhudi za
kuleta maendeleo katika mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.
0 Comments