Kagera Sukari |
Singida United Fc |
Raundi ya tano ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam
2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), utaanza Jumamosi Januari 21, 2017
kwa timu za Majimaji na Mighty Elephant za Songea kucheza kwenye Uwanja
Majimaji mjini Songea.
Ratiba ya ASFC inaonesha kwamba timu za Alliance na Mbao za Mwanza
zitacheza pia keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati Young
Africans itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es
Salaam.
Jumapili Januari 22, mwaka huu Ruvu Shooting itacheza na Kiluvya
United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Toto
Africans itacheza na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza huku Simba itakipiga na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es
Salaam kadhalika Mbeya Warriors ikicheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya.
Jumatatu Januari 23, mwaka huu Stand United itacheza na Polisi
Mara kwenye Uwanja wa Karume Mara wakati Azam itacheza na Cosmopolitan kwenye
Uwanja wa Chamazi wakati Ndanda itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona.
Jumanne Januari 24, mwaka huu Mtibwa Sugar itacheza na Polisi Moro
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Kurugenzi ya Iringa itacheza na
JKT Ruvu huko Mafinga huku Mbeya City ikipangwa kucheza na Kabela City Uwanja
wa Sokoine mjini Mbeya ilihali Madini na Panone zitacheza kwenye Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Januari 25, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na
Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mchezo mwingine
utakaozikutanisha timu za African Lyon na Mshikamano utapangiwa tarehe mpya.
Mechi hiyo imepangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru.
0 Comments