serikali imewataka watu zaidi ya 1670 katika
kaya 3331 waliovamia shamba la tanganyika packers limited
ambalo lipo katika halmashauri ya itigi mkoani Singida kuacha
kufanya shughuli za kilimo na ufugaji, mpaka uamuzi utakapo tolewa.
Naibu waziri wa kilimo ,mifugo na uvuvi William Ole Nasha ametoa tamko hilo kufuatia kukagua shamba hilo ambalo
lilimekuwa na mgongoro kati ya wananchi wa kijiji cha kitaraka
na baadhi ya watu wenye uwezo kutoka nje ya kijiji cha
kitaraka kuvamia na kuanza kulima .
kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya itigi Pius luhende amesema atahakikisha anatekeleza maagizo ya serikali mpaka
hapo uamuzi utakapo tolewa ,huku mwenyekiti wa halmashari hiyo Ally
Minja akitoa maelekezo endapo shamba lita kabidhiwa kwa halmashauri yake.
shamba la mifugo la kitaraka la kampuni ya tanganyika packers
limited lenye ukubwa wa ekari 45,000 lilianzishwa
mwaka 1955 lenye hati ya
kumiliki ardhi namba 15467 kuanzia tarehe mosi mei hadi juni
thelathini 2045 ,kwa zaidi ya miaka ishirini na
sita halitumiki kama ilivyo kusudiwa na kusababisha watu kuvamia na
kufanya shughuli za kilimo na mifugo.
0 Comments