Upinzani
wa Arsene Wenger na Jose Mourinho ni kitu cha wazi huko England kwa Miaka mingi
na Wikiendi hii watakutana tena lakini itakuwa ni mara yao ya kwanza kuvaana
tangu Mourinho awe Meneja Mpya wa Manchester United.
Jumamosi
Manchester United na Arsenal watacheza huko Old Trafford Jijini
Manchester kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Lakini
Wenger amesema tripu hiyo ya Arsenal huko Old Trafford ni Gemu tu kati ya Klabu
mbili na si Mameneja Wawili.
Akiongea
na Wanahabari hii Leo kuelekea mtanange huu wa Jumamosi, Wenger ameeleza:
“Sidhani kama napaswa kuelezea uhusiano wetu. Yeye atapigania Timu yake na mimi
nitapigania yangu. Hicho ni kitu cha kawaida!”
Aliongeza: “Siweki Gemu
hizi kama ni Mashindano kati ya Mameneja Wawili. Najua Watu wanataka
kutengeneza uhasama lakini hilo halileti Washabiki. Kitu ambacho kinavuta
Washabiki ni Gemu yenyewe na ubora wake. Ni muhimu iwe Gemu ya hali ya juu ili
kuijengea sifa Ligi Kuu. Hilo ni juu yaWachezaji
Uwanjani.”
Alipoulizwa
kama atapeana mkono na Mourinho, Wenger alijibu huku akitabasamu: “Ni wazi kitu
hicho. Naheshimu utamaduni huo kwenye Ligi Kuu.”
-Mourinho
na Wenger washapambana mara 14 kwenye Ligi Kuu England na
Wenger hajashinda hata Mechi 1.
-Mourinho, akiwa na Chelsea, ameibuka Mshindi mara 8
na Sare 6.
-Mara pekee kwa Wenger kumbwaga Mourinho ni Agosti
2015 kwenye Mechi ya kugombea Ngao ya Jamii.
Kwenye
Mechi hii ya Jumamosi, Man United itamkosa Straika wao Zlatan Ibrahimovic ambae
yupo Kifungoni Mechi 1 baada ya Kadi za Njano 5 lakini Wenger amemnyooshea
kidole Kinda Marcus Rashford ambae kwenye Mechi ya mwisho kati yao, Mwezi
Februari, alifunga Bao 2 wakati Man United inaichapa Arsenal 3-2 na kuing’oa
kwenye Reli ya kusaka Ubingwa Msimu uliopita.
Wenger
amesema: “Mtu alietuua sisi ni Rashford. Hivyo tusidhanie udhaifu wa Man
United! Msimu uliopita tulipoteza Gemu 1 tu ya Ugenini, huko Old Trafford. Na
hiyo ilikuwa Gemu muhimu kwetu na tukapoteza mwelekeo!”
-Tangu
Ligi Kuu England ianzishwe Msimu wa 1992/3, Arsenal wameshinda mara
3 tu Old Trafford katika Mechi 24.
Baada
ya Mechi 11, Liverpool ndio Vinara wakiwa na Pointi 26, Chelsea ni wa Pili wana
25, wakifuata Man City na Arsenal wenye 24 kila mmoja, Tottenham wa 5 wakiwa na
21 na Man United ni wa 6 na wana 18.
Katika
Mechi zao za mwisho za EPL kabla hawajapisha Mechi za Kimataifa, Arsenal
walitoka 1-1 na Tottenham katika Dabi ya London Kaskazini na Man United
kuitandika Swansea 3-1 huko Liberty Stadium, Wales.
0 Comments