Majengo Queens wajifua mchangani Singidani chini ya Mohamed Kweka |
Timu 12 zinatarajiwa
kushiriki Ligi ya Taifa ya Wanawake inayotarajiwa kuanza Novemba mosi, mwaka
huu kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Soka la Wanawake na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoridhia tarehe hiyo.
Tayari klabu zimeagizwa
kuzingatia jina kuenenda na namba za jezi mgongoni ili kuepusha mkanganyiko wa
wachezaji wakati wa ligi hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
Timu 12 zinatarajiwa
kushiriki ligi hiyo ambako kesho Oktoba 8, 2016 itakuwa ni siku ya kuchambua
fomu za usajili wakati Oktoba 10, mwaka huu majina ya usajili yatatangazwa
ambako pia klabu zitatumiwa kupitia anwani za barua pepe.
Oktoba 11 na 12, 2016 ni
muda wa klabu kuleta mapingamizi yatakayosikilizwa Oktoba 15, mwaka huu. Majina
ya pingamizi yatatangazwa kabla ya Oktoba 20, 2016 na maandalizi ya ligi
yataendelea.
Wakati wote huo wa
usajili, klabu hazina budi kutangaza aina ya rangi wanazotumia katika michezo
ya nyumbani na ugenini na kutakiwa kusafiri na jozi zote mbili ili kuepuka
mkanganyiko wa kufanana jezi.
Kutakuwa na jopo la
makocha watakaofanya uteuzi wa wachezaji nyota watakaoitwa kwenye timu za taifa
ambaye atagharamiwa na TFF.
Vyama vya mikoa visadie
klabu katika bajeti zao kwa vile tathamini inaonyesha kuwa fedha zinazotoka
hazitoshi. Vyama hivyo vya mikoa pia visaidie maandalizi ya michezo kama vile
kuandaa uwanja nakadhalika ukioandoa waamuzi ambao watagharamiwa na TFF.
Hakutakuwa na zawadi ya fedha zaidi ya kombe la medali kwa
timu shiriki, labda kama atatokea mdhamini mwingine. Hakutakuwa na zawadi kwa
mchezaji bora, mfungaji bora, kipa bora, ingawa kutakuwa na jopo la kuwachagua.
Mchezaji bora atachaguliwa kwenye hatua za mwisho wa mashindano, mfungaji bora
atachaguliwa kuanzia hatua ya kwanza ya mashindano.
0 Comments